Mji wa Virginia
Ramani ya Virginia

Virginia, rasmi Jumuiya ya Virginia ni jimbo la kujitawala la Marekani. Iko katika mashariki ya Marekani bara. Imepakana na West Virginia, Maryland na mkoa wa shirikisho la Washington D.C. upande wa kaskazini, North Carolina na Tennessee upande wa kusini halafu Kentucky na West Virginia upande wa magharibi. Upande wa mashariki ni bahari ya Atlantiki pamoja na hori ya Chesapeake.Mji mkuu ni Richmond (Virginia) na mji mkubwa ni Virginia Beach.

Virginia ilikuwa koloni ya Uingereza tangu kuanzishwa kwa mji wa Jamestown (Virginia) mwaka 1607. Jina la "Virginia" lamaanisha "kibikira" kwa heshima ya malkia Elizabeth I ambaye hakuolewa. Mwaka 1788 ilikuwa jimbo la kujitawala la nchi mpya ya Marekani ni moja kati ya majimbo 13 yaliyoanzisha Marekani.

Jimbo la West Virginia iliwahi kuwa sehemu ya Virginia. Wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani Virginia iliondoka katika maungano ya madola ya Marekani ikajiunga na waasi wengine katika Shirikisho la Marekani. Wakati ule wilaya kwenye magharibi ya jimbo zilijitenga na kuwa jimbo jipya lililobaki upande wa maungano hata baada ya mwisho wa vita.


Majimbo ya Marekani

Alabama Alaska Arizona Arkansas California Colorado Connecticut Delaware Florida Georgia Hawaii Idaho Illinois Indiana Iowa Kansas Kentucky Louisiana Maine Maryland Massachusetts Michigan Minnesota Mississippi Missouri Montana Nebraska Nevada New Hampshire New Jersey New Mexico New York North Carolina North Dakota Ohio Oklahoma Oregon Pennsylvania Rhode Island South Carolina South Dakota Tennessee Texas Utah Vermont Virginia Washington West Virginia Wisconsin Wyoming

Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Virginia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa .